Sera hii inaeleza jinsi tunavyokusanya, kutumia na kulinda taarifa binafsi za watumiaji wanaotumia huduma zetu za mtandaoni.
1. Ukusanyaji wa Taarifa
Tunakusanya taarifa unazotoa moja kwa moja kama:
- Jina
- Namba ya simu
- Anwani ya usafirishaji
- Barua pepe
- Taarifa za malipo (zinazosindikwa kwa njia salama bila kuhifadhi namba kamili ya kadi au maelezo ya siri)
Pia tunakusanya taarifa za kiufundi kama matumizi ya tovuti, aina ya kifaa, na kurasa unazotembelea.
2. Matumizi ya Taarifa
Taarifa zako zinatumiwa kwa:
- Kukamilisha oda na kuwasilisha bidhaa
- Kuwasiliana nawe kuhusu oda, malipo au maswali
- Kuboresha huduma na uzoefu wa mtumiaji
- Kuzuia matapeli na kuhakikisha usalama wa mifumo
3. Kushiriki Taarifa
Hatugawanyi taarifa zako kwa wahusika wengine isipokuwa:
- Watumishi au kampuni za usafirishaji ili kukamilisha oda
- Watoa huduma za malipo kwa usindikaji wa miamala
- Pale sheria inapohitaji kutoa taarifa fulani
4. Usalama wa Taarifa
Tunatumia teknolojia salama kulinda taarifa zako dhidi ya wizi, upotevu au matumizi mabaya.
Hatuifadhi taarifa nyeti za malipo kwenye mifumo yetu.
5. Vidakuzi (Cookies)
Tovuti inaweza kutumia cookies kuboresha uzoefu wa mtumiaji, kuhifadhi mapendekezo, na kufuatilia matumizi ya tovuti. Unaweza kuzima cookies kupitia kivinjari chako.
6. Haki za Mtumiaji
Una haki ya:
- Kuomba taarifa zako ulizotoa
- Kuomba marekebisho ya taarifa zisizo sahihi
- Kuomba taarifa zako zifutwe pale inapowezekana kisheria
- Kukataa matumizi ya taarifa kwa madhumuni ya masoko
7. Mabadiliko ya Sera
Sera hii inaweza kubadilishwa wakati wowote. Mabadiliko mapya yatatangazwa kwenye ukurasa wa sera ya faragha.
8. Mawasiliano
Kwa maswali au maombi kuhusu taarifa zako, wasiliana nasi kupitia namba ya simu au barua pepe iliyo kwenye ukurasa wetu wa mawasiliano.